0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Serikali imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa iliyotolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) na kusambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuhusu siku 100 za utawala wa Rais Magufuli kuwa zimekandamiza Uhuru wa Habari nchini kwa kulifuta Gazeti la Mawio.

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inasisisitiza kwamba hatua iliyochukuliwa dhidi ya gazeti la Mawio ni Sahihi na lilistahili adhabu hiyo. Aidha, taratibu zote za kulifuta Gazeti hilo zilifuatwa ikiwa ni pamoja na Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo kupewa nafasi ya kujitetea.
Hatua ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRCD) kutaka kujenga taswira kwamba Gazeti la MAWIO lilionewa na kwamba halikupewa nafasi ya kujieleza na kujitetea si sahihi na ni kuupotosha umma.

Serikali inazitaka taasisi zinazo jishughulisha na Utetezi wa Haki za Binadamu kuacha kufanya tafsiri potofu kwa Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976 na Sheria nyingine za nchi. Hakuna Uhuru usio na Mipaka na Staha.

Serikali inautaarifu Umma kuwa hatua ya kutunga Sheria ya Huduma za Habari (Media Service Bill) na Haki ya kupata tarifa inaendelea vizuri na Wizara zinaendelea kupokea maoni ya kuboresha Miswaada hiyo.

Muswaada wa Haki ya Kupata Taarifa unasimaiwa na Wizara ya Katiba na Sheria, Muswaada huo unawahusu watu wote. Muswaada wa Huduma za Habari ni mahsusi kwa Wadau wote wa tasnia ya Habari.

Serikali inatoa wito kwa wadau wote wa sekta ya habari kuchangia kuboresha miswaada hiyo. Aidha, inawataka Wanahabari wawe mstari wa mbele katika kuchangia uboreshaji wa Muswaada wa Huduma za Habari badala ya kuwaachia wanataaluma nyingine kutoa maoni na maelekezo katika muswaada huo.

Serikali inawakumbusha wananchi kwamba Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 itaendelea kutumika mpaka pale Sheria mpya itakapopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika hatua nyingine Serikali inapenda kuwataarifu wananchi kuwa suala la urushaji wa matangazo ya “live” kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) lilisha tolewa ufafanuzi na Viongozi Wakuu wa Serikali. Hivyo mjadala huo ulihitimishwa.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO)

Post a Comment

 
Top