CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewataka wananchi kutohofia vitisho vilivyopangwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salam unaotarajiwa kufanyika kesho,
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Saalam Salim Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Chadema amesema, zipo tetezi kwamba CCM wamepanga kufanya fujo katika uchaguzi huo ili kupora ushindi wa Chadema.
Amesema, licha ya wajumbe wa vyama vinavounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kuwa wengi kuliko wa CCM, bado serikali kwa kushirikiana na CCM wamepania kukamata wajumbe wa UKAWA ili kupunguza idadi ya wapiga kura.
Nakwamba, kutokana na kikao kilichokaliwa wiki iliyopita kikiwajumuisha wajumbe wanasiasa kutoka vyama vyote vya upinzani (UKAWA) kiliazimia, washiriki watakao shiriki kumchagua meya ni wale tu waliowachagua mameya wa Manispaa, hivyo wajumbe toka Zanzibar hawataruhusiwa kupiga kura.
“Jumla ya wajumbe ni 161 kwa jiji zima la Dar es Salaam ambapo, kwa upande wa Kinondoni kuna wajumbe 58 ambapo CCM wapo 20 na ukawa 38, Temeke jumla ya wajumbe 49, CCM wapo 31 na ukawa 18 na Ilala jumla ya wajumbe 54 huku CCM wakiwa 23 ukawa 31. Ni dhairi kuwa tumewashinda ila hawataki kukubali na kuachia madaraka,” amesema Mwalimu.
Pia amesema, CCM wanampango wa kuvunja la Dar es Salaam kwa kisingizio kuwa madiwani na wabunge wameshindwa kupiga kura, kwa hivyo wanampango wa kuunda Tume ya Jiji itakayokuw chini yao.
“Nitoe wito kwa wananchi, watakaohudhuria uchaguzi wa kesho wawe makini, kwani kunampango wa CCM kuwaleta maaskari wengi wenye silaha ili kuwatishia wananchi wenye haki ya kushiriki.”
Post a Comment