MIMBA ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu inazidi kuzua ya kuzua kila kukicha baada ya hivi karibuni, Mshindi wa Big Brother Africa Hot Shots 2015, Idriss Sultan ambaye anajigamba kuwa ndiye mwenye ujauzito huo kupachikwa jina la Dk. Mwaka.
Idriss amepewa jina hilo kwa vile Tabibu wa Tiba Mbadala Tanzania, Juma Mwaka Juma JJ Mwaka au ‘Dk. Mwaka’ amekuwa akisifika kwa kuwatibu wanawake wenye matatizo ya kutoshika mimba.
Mitandao mbalimbali ya kijamii wiki iliyopita ilimwita Idriss ni Dk. Mwaka huku ikimsifia kuwa, wameshindwa wanaume wengi, akiwemo Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aliyewahi kuwa mpenzi wa Wema lakini yeye ameweza kumpa furaha mrembo huyo kwa kumpachika ujauzito.
“Kweli wewe Idriss ni Dk. Mwaka. Maana Mwaka amekuwa akiwasaidia wanawake kupata watoto. Wema ametoka na wanaume kibao, lakini wewe dogo umeweza, big up!” ulisomeka mtandao mmoja.
Gazeti hili lilimtafuta Dk. Mwaka kwa njia ya simu ili kumuuliza amelichukuliaje tukio la Idriss kuitwa kwa jina lake.
“Pengine uwezo wangu wa kazi umesababishwa aitwe hivyo. Lakini mimi bado nabaki kuwa Dk. Mwaka orijino na kazi yangu inajulikana,” alisema Dk. Mwaka.
Idriss hakupatikana hewani juzi kuzungumzia ishu hiyo lakini kwa nyakati tofauti amewahi kucheka tu kwa watu kumwita jina hilo.
Post a Comment