0
Msanii wa filamu Vincent Kigosi ‘Ray’ baada ya kuchanwa kwenye wimbo wa Nay wa Mitego ‘Shika Adabu Yako’ kuwa bado anaishi kwao, amejibu tuhuma hizo kwa kudai anaishi kwao mpaka sasa ili kuwa karibu na Mama yake.

Akizungumza katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Ijumaa hii, Ray alisema yeye ni mtoto wa mwisho hivyo anahitaji kuwa karibu zaidi na Mama yake.

“Ni kweli naishi nyumbani na kuishi kwetu sio kama sina nyumba, na kuishi nyumbani sio dhambi. Uwezo wa kupanga ninao lakini mama yangu hapendi nihame nyumbani kwetu ,” alisema Ray.

“Kujitegemea ni maamuzi yako binafsi, mimi naishi nyumbani na mama yangu ni mtoto wa mwisho lakini huwa sipendi kujionyesha nina utajiri gani?, Sipendi kupost mali zangu, sinina nyumba, magari ni ishu zangu binafsi, kila msanii ana style yake ya maisha, mwingine anapenda kujionyesha kwenye mitandao ana mali gani,” aliongeza Ray.

Pia Ray alisema yeye na mpenzi wake Chuchu Hans kila mtu anaishi kwake.

“Mpenzi wangu anaishi kwake na mimi naishi nyumbani kwetu. Mama yangu alishaniambia hata nikihama atakuja kuishi na mimi nyumbani kwangu. Chuchu Hans anajua kuhusu hili hata nyumba anayoishi nimempangia mimi,” alisema Ray.

Post a Comment

 
Top