0
Nimeshangazwa kidogo kwa kitendo cha Rais Dkt Magufuli kuwaandalia karamu ya kuukaribisha mwaka mpya, mabalozi na Maafisa wa kimataifa waliopo nchini na kisha yeye mwenyewe kumtuma waziri wake wa mambo ya nje kumwakilisha.

Kwa maoni yangu naamini hili ni kosa la kiufundi hasa ikizingatiwa kuwa Magufuli ndio ameanza tenure yake kama Raisi na hivyo angepaswa kutumia fursa hiyo kikamilifu ili kujenga taswira yake vema kimataifa kupitia kile anachokiamini na kusimamia.

Taarifa iliyorushwa na vyombo vya habari haikusema ni dharura gani aliyokuwa Mhe Rais ilihali yupo nchini.\

Source:Jamii Forums

Post a Comment

 
Top