Wakili wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Wakili Msomi Awadh Ali amesema kuwa uchaguzi wa marudio wa Zanzibar haupo kisheria. Wakili Awadh,akihojiwa na ITV,amesema kuwa Katiba na Sheria ya Uchaguzi wa Zanzibar haitambui uchaguzi wa marudio.
Wakili Awadh amesema kinachofanywa na ZEC ni kuwashurutisha wanasiasa na wananchi kushiriki kwenye uchaguzi wa marudio hapo Machi 20. Wakili Awadh amesema kuwa washindi wa uchaguzi wa mwaka jana walishapewa vyeti vya ushindi na hivyo hawawezi kupokwa vyeti vyao.
Kuhusu pendekezo la kukimbilia mahakamani kupinga uchaguzi wa marudio,Wakili Awadh amesema kuwa Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar pamoja na Katiba haziruhusu kupingwa au kuchunguza ZEC kimahakama.
Post a Comment