0
Baada ya maneno ya muda mrefu na shutuma kwenda kwa tume kuwa "imeufuta" uchaguzi bila kufuata taratibu,hatimaye Tume imekuja na ushahidi wa nyaraka za form namba MUR.12A zinazoonyesha jinsi hujuma ilivyofanywa kuuvuruga uchaguzi na hivyo kupelekea uchaguzi kuwa "batili" na hatimaye kuipa ZEC mamlaka ya kisheria ya kuufutilia mbali uchaguzi huo.Mwenyekiti wa ZEC ndugu Jecha S Jecha aliuthibitishia umma kuwa uchaguzi wa mwaka 2015 uligubikwa na ukiukwaji mkubwa wa kanuni,taratibu na sheria za uchaguzi na hivyo kuufanya kuwa batili.

Ubatili wa uchaguzi huo unaopaswa kurudiwa 20/03/2016 umezidi kuanikwa kwa ushahidi wa nyaraka za form za uchaguzi.Kwa mfano katika kituo cha Skuli ya Mabaoni #23801 Jimbo la Chonga namba 2909 form ya matokeo ya uchaguzi haina muhuli wa tume,hii ni sababu ya kufanya matokeo haya kuwa batili na haramu.Pia katika kituo cha Gamba #2008 form ya matokeo ya uchaguzi imefutwafutwa kwa juu na hivyo kusababisha majina na tarakimu kutoonekana kwa uzuri,hali hii pia inaleta ubatili na uharamu wa matokeo na hatimaye kutia doa uchaguzi wenyewe.

Katika kituo cha Mwembe Makumbi #21618 Jimbo la Chumbuni form ya matokeo imefutwafutwa na kupandikiza majina ya mawakala wengine ambao hawakuwepo wala kuhudhuria ktk eneo(kituo) cha uchaguzi,hii ni sbb nyingine amabayo inaipa ZEC nguvu za kubatilisha uchaguzi huu na kuamuru urudiwe 20/03/'16.Kiwanja cha Mpira Masumbani katika Jimbo la Chumbuni,kituo hicho matokeo yake ni batili sababu yameandikwa tena kwa kalamu juu ya maandishi ya kivuli na saini imewekwa zaidi ya mara moja,katika Jimbo la Chake Chake Pemba,form katika kituo cha kupigia kura jina la kituo halionekani na namba haisomeki na form imepigwa muhuli wa Serikali ya Mapinduzi ya Z'bar badala ya muhuli wa ZEC.Eneo kubwa katika vituo vya uchaguzi kisiwa cha Pemba,mihuli na majina mengi yameghushiwa kama yanavyoonekana katika form hizi zilizoambatanishwa.

Kwa sababu hizo,na nyinginezo nyingi kama za wajumbe wa tume kupigana,uchaguzi huu ulikuwa batili na wala ZEC isingeweza kutangaza matokeo sababu kungezuka vurugu zisizokuwa na maana.Hivyo kwa ushahidi huu wa nyaraka za form za uchaguzi Z'bar kuwa na mapungufu,Tume ya uchaguzi Zanzibar iliona hujuma hii na kuamuru uchaguzi huo kurudiwa

Post a Comment

 
Top