Breaking News:Mbunge wa Zamani wa Nyamagana Ezekiel Wenje Apata Ajali ya Gari
Gari lililokuwa likiendeshwa na aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje limepata ajali maeneo ya Magereza Bariadi mkoani Simiyu mchaba wa leo baada ya kuacha njia na kugonga mtaro na kisha kuanguka. Ndani ya gari hilo alikuwepo pia Mbunge wa VIti Maalumu (Chadema), Gimbi Masaba na Mwandishi wa habati wa Tanzania Daima, Sitta Tuma ambao wamepata michubuko kidogo.
Post a Comment