Msanii wa muziki wa R&B Benard Paul ‘Ben Paul’, amesema hapendi kuchora tattoo, kuvaa hereni pamoja na kusuka rasta kama baadhi ya wasanii wanavyofanya kwa kuwa ana uheshimu sana mwili wake.
ben-pol
Akizungumza na gazeti la Mtanzania, Ben Paul alisema imekuwa ni kawaida kwa idadi kubwa ya wasanii kujichora ‘tattoo’ na kuwa na mwonekano wa tofauti na watu wengine, lakini kwake jambo hilo halina nafasi.
“Japo ni msanii lakini sipendi kuwa na mwonekano wa tofauti kama kufuga rasta, kuvaa hereni au kujichora mwilini kwa sababu nauheshimu mwili wangu, ndiyo maana nipo kawaida kila wakati,” alisema Ben Pol.
Ben Pol na Jux hivi karibuni wameachia wimbo wao mpya uitwao ‘Nakuchana’.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment