0
Baba wa staa wa muziki Diamond Platnumz, Abdul Juma amedai Wema Sepetu ndiye mwanamke pekee ambaye mwanae Diamond aliweza kumtambulisha kwake kama mpenzi wake.

Akizungumza katika kipindi cha The Weekend Chat Show cha Clouds TV, Mzee Abdul alidai Diamond alimtambulisha Wema kwake pamoja na kumvalisha pete.

“Yaani Diamond toka akiwa na Wema ndio alikuja hapa kumvalisha pete Wema,” alisema Mzee Abdul.

“Unajua toka nizaliwe sijawai kuona mwanamke mwenye heshima zake kama Wema. Nimewai kuletewa mwanamke mmoja tu toka (Diamond) anakuwa,”. Alisema

Aliongeza, “Only one hana umalaya huo. Kwa sababu mimi Diamond namwamini kitu kimoja, muda wakutembelea kwenye madisko hana. Yeye ni mtu wa kukaa nyumbani na kufikiria anafanya nini kwa sababu mwenyewe anajiona yupo kwenye ushindani, bila kujiandaa kwa ajili ya kazi zijazo ‘atarostika’. Kwahiyo mimi nasema big up akaze buti,”

Post a Comment

 
Top